Tanzanian loan officer handing a stack of money to a smiling woman with one hand, while shaking her hand with the other, symbolizing successful loan disbursement and trust.

Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Ya Microfinance

NINI MAANA YA BIASHARA YA MICROFINANCE?

Hebu fikiria watu wenye biashara ndogo ndogo, kina mama wa nyumbani na baadhi ya watu wanaopata dharura za haraka za kifedha na wanashindwa kupata mikopo kutoka kwenye benki kubwa kwa sababu ya kutotimiza vigezo na masharti wanapata wapi fedha?

Ili kuwasaidia watu wa namna hii waweze kupata mikopo ndio watu mbali mbali hujitokeza na kuwakopesha mikopo midogo midogo mara nyingi chini ya milioni hamsini (50). Hii aina ya kukopesha watu wa namna hii ndio inaitwa biashara ya microfinance.

HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA YA KUKOPESHA (MICROFINANCE)

Hatua hizi zitakusaidia kuweza kuanzisha biashara ya microfinance nchini Tanzania;

1. FANYA UTAFITI WA SOKO LA BIASHARA YAKO

Kabla ya kuanzisha biashara yako ya microfinance, ni muhimu kufanya utafiti wa kina wa soko. Utafiti huu utakusaidia kuelewa mahitaji ya wateja wako, ushindani uliopo, na fursa za ukuaji. Chunguza ni aina gani ya huduma za microfinance zinazohitajika katika eneo unalolenga, ni nani washindani wako, na ni nini kinachowafanya wateja wachague taasisi moja kuliko nyingine. Taarifa hizi zitakusaidia kuunda mkakati wa biashara uliofanikiwa na kuepuka makosa ya gharama kubwa baadae.

2. TAFUTA MTAJI WA BIASHARA

Baada ya kukamilisha utafiti wa soko, hatua inayofuata ni kutafuta mtaji wa biashara. Mtaji ni muhimu kwa ajili ya gharama za uanzishaji, uendeshaji, na ukuaji wa biashara yako. Fanya tathmini ya mahitaji yako ya kifedha na uchunguze vyanzo mbalimbali vya mtaji kama vile akiba binafsi, mikopo kutoka taasisi za fedha, ruzuku, au wawekezaji.

3. SAJILI JINA LA BIASHARA AU KAMPUNI YAKO BRELA

Hatua ya kwanza ni kusajili jina la biashara au kampuni yako kwa wakala wa usajili wa majina ya biashara na leseni (BRELA) ambapo baada ya usajili utapewa cheti cha usajili wa jina la biashara au kampuni yako. Hapa taarifa muhimu zinazohitajika ni jina la biashara au kampuni, namba za utambulisho wa taifa wa wamiliki na mawasiliano yao.

Kwa mujibu wa sheria jina la biashara la microfinance inatakiwa liwe na moja wapo ya haya maneno: Microfinance, Microcredit, Financial services, Finance au Credit. Hivyo hakikisha unaposajili BRELA jina lako linakidhi hitaji la kisheria la jina la biashara.

4. PATA T.I.N YA BIASHARA PAMOJA NA CHETI CHA MALIPO YA KODI)

Baada ya kupata usajili kutoka Brela, unatakiwa Kwenda Mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) ukiwa pamoja na nyaraka zako za usajili kutoka BRELA kwa ajili ya kupata namba ya mlipa kodi (T.I.N) inayosoma jina la biashara au kampuni yako Pamoja na kupewa Tax clearance certificate.

5. PATA KIBALI CHA KUKOPESHA FEDHA KUTOKA BENKI KUU (B.O.T)

Ukishakamilisha hatua ya Brela pamoja na TRA, sasa ni wakati wa kwenda Benki Kuu (BoT) ili kupata kibali cha kukopesha fedha (microfinance), kumbuka bila kibali hiki huwezi kupewa leseni ya biashara ya microfinance.

Katika hatua hii baadhi ya viambatanisho utavotakiwa kuwa navyo ni: Nyaraka za usajili kutoka Brela, TRA, CV za wamiliki, nakala za vyeti vya taaluma na vitambulisho vya taifa vya wamiliki, sera ya ukopeshaji, benki statementi yenye kuonesha mtaji wa biashara, sampuli ya fomu na mkataba wa ukopeshaji fedha wataotumia wateja wako.

6. PATA LESENI YA BIASHARA YA MICROFINANCE

Hii ni hatua ya mwisho usajili wa biashara ya microfinance, leseni ya biashara ya kukopesha fedha (microfinance) hutolewa na BRELA. Nyaraka unazotakiwa ambatanisha hatua hii ni vyeti vya usajili wa jina la biashara au kampuni, T.I.N ya biashara, tax clearance, nakala za vitambulisho vya taifa vya wamiliki Pamoja na kibali cha kukopesha fedha ulichokipata Benki Kuu Ya Tanzania (B.O.T).

7. ANDAA OFISI NA WAFANYAKAZI

Baada ya kusajili kampuni, andaa ofisi inayokidhi mahitaji ya biashara yako na kuvutia wateja. Chagua eneo lenye urahisi wa kufikika na linaloendana na hadhi ya biashara yako. Vile vile, tafuta wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu katika sekta ya microfinance, hasa katika maeneo ya mikopo, fedha, na huduma kwa wateja. Wafanyakazi bora watasaidia kuendesha biashara kwa ufanisi na kujenga uhusiano mzuri na wateja.

8. ANZA KUITANGAZA OFISI

Mara baada ya kuanzisha biashara yako ya microfinance, ni muhimu kuanza kuitangaza ili kuwafikia wateja wengi zaidi. Tumia mbinu mbalimbali za matangazo kama vile matangazo kwenye mitandao ya kijamii, tovuti, vipeperushi, na matangazo kwenye redio au televisheni. Eleza faida za huduma zako na jinsi zinavyoweza kuwasaidia wateja kufikia malengo yao ya kifedha. Jenga uhusiano mzuri na jamii na ushiriki katika matukio ya kijamii ili kuongeza uaminifu na kujulikana kwa biashara yako.

🧭 UNAHITAJI MSAADA KUSAJILI BIASHARA YA MICROFINANCE?

Tunajua kuwa mchakato wa kupata leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) unaweza kuwa mgumu na kuchukua muda — ndiyo maana tumekuandalia njia mbili za kukusaidia:

✅ Chaguo la 1: Tuachie Tushughulikie Kwa Niaba Yako

Ikiwa unahitaji msaada kamili wa usajili wa Microfinance, tunaweza kukusaidia kufanya kila kitu kwa niaba yako — iwe ni kuanzia usajili wa kampuni BRELA, au ni kuanzia kufuatilia leseni ya Microfinance pekee kutoka BoT.

Tutakuandalia nyaraka zote, tutatuma maombi rasmi, na kufuatilia hadi upate leseni yako kikamilifu. Gharama ya huduma ya kufuatilia leseni ya Microfinance BOT ni TZS 349,000 tu, Hii ni kwa wale ambao wameshakamilisha hatua za usajili za mwanzo BRELA & TRA, kama bado tutakupa gharama za kuanzia hatua ya kwanza.


📘 Chaguo la 2: Fanya Mwenyewe kwa Mwongozo Wetu wa PDF

Unapendelea kufanya mwenyewe kwa hatua zote za usajili wa Microfinance?
Pata Package Yetu Ya Mwongozo Wa Usajili Wa Microfinance Kwenye mfumo wa PDF kwenye email/whatsapp yako — Mwongozo utaweza ku-download ukiwa na mambo yafuatayo ndani:

✅ Orodha kamili ya mahitaji
✅ Templates zinazoweza kuhaririwa (Word/PDF)
✅ Maelezo ya hatua kwa hatua jinsi ya kuomba leseni
✅ Vidokezo vya kitaalamu vya kuepuka kukwama

🛒 Nunua Mwongozo Huu Sasa kwa TZS 99,000 TU.


💬 Hitimisho

Haijalishi kama unahitaji msaada wa kitaalamu au unataka kujisaidia mwenyewe — jambo muhimu ni kuchukua hatua sahihi mapema. Usikose fursa ya kuanzisha biashara ya microfinance kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria.

Imeandaliwa na :
Charles Mwegalawa
Mtaalamu Masuala Ya Usajili Wa Biashara,
V.A Business Consultants
May 2025

Scroll to Top