Memorandum & Articles Of Association Ni Nini?
Memorandum and articles of asssociation (MEMART) ni nyaraka rasmi ya kisheria inayoeleza kwa undani muundo wa kampuni, uhusiano wake na umma, haki na wajibu wa wanahisa pamoja na wakurugenzi, na jinsi kampuni inavyopaswa kuendesha shughuli zake kisheria.
Umuhimu Wa Memorandum & Articles Of Association
Bila MEMART, huwezi kusajili kampuni yako BRELA kwani ndio nyaraka kuu inayotambulisha muundo, kanuni na masharti ya kampuni. Ni nyaraka inayohitajika kisheria, na makosa madogo yanaweza kufanya usajili wako uchelewe au kukataliwa.
Taarifa Muhimu Tunazohitaji Ili Kuandaa MEMART:
Unapojaza fomu ya maombi ya Memart, utatupa taarifa rahisi kuhusu:
1. Jina la Kampuni – jina rasmi la kampuni lililosajiliwa.
2. Aina ya Kampuni – kama ni Private Limited au Public Limited
3. Shughuli za Biashara – lengo kuu la kampuni na huduma au bidhaa zinazotolewa.
4. Wamiliki / Wakurugenzi – majina, taifa na idadi ya wamiliki au wakurugenzi.
5. Anuani ya Usajili – anuani rasmi ya kampuni kwa malengo ya kisheria (kama ipo)
6. Maelezo Zaidi (hiari) – masharti maalumu au taarifa nyingine muhimu kwa uendeshaji wa kampuni.
Kwanini Tunatoa Huduma Ya Memart
Watu wengi wanaojaribu kusajili kampuni zao wenyewe kupitia BRELA ORS hukutana na changamoto kubwa kwenye hatua ya kuandaa na kuwasilisha MEMART.
Makosa madogo kwenye MEMART yanaweza kuwalazimisha wateja kulipa gharama kubwa za marekebisho au kuendelea kuchelewa kwenye usajili wa kampuni zao sababu ya MEMART zao kukataliwa na BRELA.
Hapa ndipo tunapokuja — V.A Business Consultants tunakuandalia MEMART sahihi na ya kisheria ambayo unaipata ndani ya siku moja tu kwa gharama ya TZS. 99,000 Tu. Memart hii itakusaidia kusajili kampuni yako kitaalamu, haraka na bila makosa. Ni ushirikiano rahisi na win-win kwa wote.
Je, Uko Tayari Kupata Memart Yako?
Jaza fomu kwenye kurasa hii sasa hivi na timu yetu itakuandalia MEMART yako haraka, ili usajili wa kampuni yako kupitia BRELA ukamilike bila vikwazo.
Omba Memart Yako Sasa
Jaza fomu hii na kisha lipa mtandaoni. Tutatengeneza Memart yako na kukutumia ndani ya 24–48 saa.