Jinsi Ya Kusajili Jina La Biashara Tanzania 2025

JINSI YA KUSAJILI JINA LA BIASHARA TANZANIA

Usajili wa jina la biashara ni hatua muhimu kwa wajasiriamali na wawekezaji nchini Tanzania. Ikiwa unataka kuendesha biashara kwa jina rasmi, usajili kupitia BRELA ni hatua ya kwanza ya kisheria unayopaswa kuchukua.

Kwa Nini Usajili wa Jina la Biashara ni Muhimu?

  • Unapata utambulisho halali wa kibiashara
  • Unaweza kufungua akaunti ya benki ya biashara
  • Huwezesha kuingia mikataba kisheria
  • Ni hitaji la kisheria kwa biashara nyingi

Hatua za Kusajili Jina la Biashara

Zifuatazo ni hatua kuu:

  1. Chagua Jina: Hakikisha jina lako ni la kipekee na halijatumika.
  2. Sajili Jina La Biashara yako: Tembelea tovuti ya ORS ya BRELA.
  3. kisha tuma maombi ya usajili wa jina la biashara
  4. Lipia Ada: Malipo hufanyika kwa njia ya mtandao (GePG).
  5. Pata Cheti Cha Usajili: Kama ombi la usajili limekubaliwa utapewa cheti cha usajili wa jina la biashara, na kama halijakubaliwa utaambiwa changamoto ya ombi lako ni nini urekebishe kisha utume maombi tena.

Muda Gani Inachukua?

Mara nyingi ndani ya siku 1 hadi 3 za kazi kama hakuna pingamizi au tatizo kwenye jina lililochaguliwa.

Baada ya Usajili, Nifanye Nini?

Baada ya kupata cheti, unaweza kuendelea na hatua nyingine muhimu kama kupata:

  • TIN (Namba ya Mlipa Kodi)
  • Leseni ya biashara kutoka Halmashauri
  • Kufungua akaunti ya biashara nk.

Unahitaji Msaada Kusajili Jina la Biashara?

V.A Business Consultants ni wataalamu wa usajili wa majina ya biashara, kampuni, na vibali vyote vya biashara Tanzania.

Tupo tayari kukusaidia haraka na kwa usahihi — iwe uko Dodoma au popote Tanzania.

📞 Piga: 0759 001 212
💬 WhatsApp: Bofya Hapa

Anza Usajili Sasa

Scroll to Top