🚀Anza Usajili Wa Biashara Yako

Chagua hapa chini unahitaji kuanza usajili wa kampuni au jina la biashara yako – Tutakua nawe kila hatua.

Usajili Wa Kampuni

Chaguo Bora kwa Biashara Zinazokua au Zenye Malengo Makubwa. Inatoa ulinzi wa kisheria, uaminifu wa kibiashara, na fursa ya kupanuka kitaasisi.

Usajili Wa Jina La Biashara

Nzuri kwa biashara ndogo au zinazomilikiwa na mtu mmoja. Ni rahisi, haraka, na nafuu — njia bora ya kuanzisha rasmi biashara yako.

🔍 Jinsi Ya Kuanza Usajili

Chagua unaanza usajili wa kampuni au wa jina la biashara

Jaza taarifa za biashara yako kupitia mfumo wetu wa kupokea taarifa ulio salama na wa uhakika

Ukishaza fomu ya taarifa, utazituma taarifa zako kwetu kwa ajili ya kufanyiwa kazi

💳 Lipa kwa Usalama kwa kutumia Simu (Mobile Money), Benki, au Kadi (usajili huanza mara moja) — au chagua kuzungumza na mshauri wetu kwanza kupitia WhatsApp.

📝 Tunaandaa na kuwasilisha nyaraka zote BRELA kisha tunafuatilia hadi upate nyaraka za usajili.

📬 Mara baada ya usajili kukamilika, tunakutumia cheti chako kupitia barua pepe, WhatsApp au nakala halisi.

✅ Uko Tayari Kuanza Usajili?

Wataalamu wetu wapo tayari kukusaidia kila hatua utayokua unapita

💬 Maswali Yaulizwayo Mara Kwa Mara

🏢 Jina la Biashara ni njia rahisi na nafuu ya kuanzisha biashara, lakini Kampuni inatoa uaminifu zaidi, ulinzi wa kisheria, na fursa ya kukua kwa haraka.

Kawaida ni siku 1-3 baada ya kupokea taarifa na malipo yako.

🆔 Unachohitaji ni NIDA yako na maelezo machache ya biashara.

💳 Unaweza kulipa kwa usalama kupitia njia yetu ya malipo online (kwa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa au kadi), au chagua kuzungumza na mshauri wetu kwanza whatsapp kabla ya malipo. Tunatoa njia rahisi na rafiki kwako.

Tutakutumia cheti chako cha usajili pamoja na nyaraka zote kupitia barua pepe (email) na WhatsApp mara tu usajili utakapokamilika. Ikiwa unapendelea, tunaweza pia kupanga kukuletea nakala halisi (hardcopy).

Ndiyo! Tunatoa msaada wa huduma za baada ya usajili kama vile usajili wa TIN (TRA), leseni ya biashara, vibali mbalimbali (kama NSSF, WCF) pamoja na huduma za kuhakikisha biashara yako inabaki salama kisheria na kufuata taratibu zote za kisheria.

💰 Kwa bei ya huduma, tafadhali angalia kurasa zetu za Usajili wa Jina la Biashara na Usajili wa Kampuni.

💡 Kumbuka: Sisi ni kampuni binafsi ya ushauri inayosaidia katika mchakato wa usajili wa biashara kupitia BRELA na taasisi nyingine muhimu. Jukumu letu ni kuandaa nyaraka zote, kuzifikisha mahali husika, kufuatilia hatua kwa hatua, na kukupa msaada kamili hadi usajili ukamilike.

Scroll to Top